Mdogo kuliani na mkubwa kushoto – nani aanze kumuhudumia?

Swali: Vipi ikiwa aliye upande wa kulia ni mdogo na aliye upande wa kushoto ndiye mkubwa?

Jibu: Amuombe idhini. Vinginevyo ampe aliye upande wa kulia hata kama ni mdogo. Kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa Ibn ´Abbaas kinywaji na akawaacha watuwazima. Isipokuwa ikiwa atamuomba idhini yule mdogo aliye upande wa kulia kwamba awape walioko upande wa kushoto. Katika hali hiyo hapana vibaya.

Swali: Katika kikao aanze na mkubwa au upande wa kulia akiingia na udi na chai?

Jibu: Aanze na kiongozi wa kikao. Aanze na yule mkubwa kisha ampe aliye upande wa kulia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23247/حكم-البدء-بمن-على-اليمين-لو-كان-صغيرا
  • Imechapishwa: 11/12/2023