Kumsengenya mtu ambaye hatambuliwi kwa msimuliwaji

Swali: Anayemsengenya mtu ambaye hajulikani kwa yule msikilizaji au akamtaja jina lake lakini msikilizaji hamjui?

Jibu: Hata kama. Usengenyi haujuzu:

وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا

“Na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo.”[1]

Haijuzu muda wa kuwa kamtaja.

Swali: Akisema ´watu wa mji fulani` au ´wengi wa watu` inazingatiwa kuwa usengenyi?

Jibu: Asiyetambulika haizingatiwi ni usengenyi. Ukisema ´baadhi ya watu wanafanya hivi, baadhi ya wanaume wanafanya hivi` hauzingatiwi ni usengenyi.

[1] 49:12

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23253/هل-تجوز-غيبة-رجل-غير-معروف-للسامع
  • Imechapishwa: 11/12/2023