04. Hadiyth “Kulitajwa mbele ya Mtume wa Allaah kitunguu saumu… “

334 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kulitajwa mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kitunguu saumu, kitunguu maji na figili, kukasemwa: “Ee Mtume wa Allaah, mbaya zaidi katika yote hayo ni kitunguu saumu. Je, unaiharamisha?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

كلوه، مَن أكله منكم فلا يقربْ هذا المسجدَ، حتى يذهبَ ريحُه منه

“Kuleni, lakini yule katika nyinyi atakayevila basi asikurubie msikiti huu mpaka imwondoke harufu yake.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/255)
  • Imechapishwa: 11/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy