Abu ´Abdir-Rahmaan Muhammad bin al-Husayn bin Muusa as-Sulamiy ametukhabarisha: Muhammad bin Mahmuud al-Faqiyh al-Marwaziy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Umayr ar-Raaziy ametuhadithia: Abu Zakariyyaa Yahyaa bin Ayyuub al-´Allaaf at-Tujiybiy ametuhadithia huko Misri: Yuunus bin ´Abdil-A´laa ametuhadithia: Ash-hab bin ´Abdil-´Aziyz ametuhadithia: Nimemsikia Maalik bin Anas akisema:

”Tahadharini na Bid´ah!” Ikasemwa: ”Ee Abu ´Abdillaah, Bid´ah ni kitu gani?” Akasema: ”Wazushi ni wale wanaozungumza juu ya majina ya Allaah, sifa, maneno, ujuzi na uwezo Wake na hawayanyamazii yale yaliyonyamaziwa na Maswahabah na wale wanafunzi wao.”

Abul-Husayn Ahmad bin Muhammad bin ´Umar az-Zaahid al-Khaffaaf ametukhabarisha: Abu Nu´aym ´Abdul-Malik bin Muhammad bin ´Adiy al- ametukhabarisha: ar-Rabiy´ bin Sulaymaan ametukhabarisha: Nimemsikia ash-Shaafi´iy akisema:

”Inanipendeza zaidi mja akutane na Allaah akiwa na madhambi yote, isipokuwa tu shirki, kuliko kukutana naye akiwa na kitu katika matamanio.”

Abut-Twaahir Muhammad bin al-Fadhwl amenikhabarisha: Abu ´Amr al-Hayriy ametuhadithia: Abul-Azhar ametuhadithia: Qabiyswah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin Burqaan, aliyesema:

”Bwana mmoja alimuuliza ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz juu ya kitu katika matamanio, ambapo akasema: ”Lazimiana, ee mtoto, na dini ya Qur-aan na mabedui na achana na mengine yote yasiyokuwa hayo.”

Abu ´Abdillaah al-Haafidhw ametukhabarisha: Muhammad bin Yaziyd ametuhadithia: Nimemsikia Abu Yahyaa al-Bazzaar: Nimemsikia al-´Abbaas bin Hamzah: Nimemsikia Ahmad bin Abiyl-Hawaariy: Nimemsikia Sufyaan bin ´Uyaynah akisema:

”Yale yote ambayo Allaah amejisifu kwayo ndani ya Kitabu Chake tafsiri yake ni kule kuyasoma na kuyanyamazia.”

Abul-Husayn al-Khaffaaf ametukhabarisha: Abul-´Abbaas Muhammad bin Ishaaq as-Sarraaj ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Abiyl-Haarith ametuhadithia: al-Haytham bin Khaarijah ametuhadithia: Nimemsikia al-Waliyd bin Muslim akisema:

”Nilimuuliza al-Awzaa´iy, Sufyaan na Maalik kuhusu Hadiyth zinazoongelea Sifa na Kuonekana. Wakasema: ”Zipitisheni kama zilivyokuja pasi na namna.”

Imaam az-Zuhriy, ambaye alikuwa imamu wa maimamu na kito cha wanazuoni katika wakati wake, amesema:

”Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, ni jukumu la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufikisha na jukumu letu ni kujisalimisha.”

Baadhi ya Salaf wamesema:

”Hakuna mtu anayepata uimara ndani ya Uislamu isipokuwa kwa kujisalimisha.”

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 242-250
  • Imechapishwa: 12/12/2023