Abu Twaahir bin Khuzaymah ametukhabarisha: Babu yangu imamu ametuhadithia: Ahmad bin Naswr ametuhadithia: Abu Ya´quub al-Hunayniy ametuhadithia: Kathiyr bin ´Abdillaah al-Muzaniy ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika dini hii ilianza ngeni na itarudi kuwa ngeni kama ilivyoanza – Twubaa kwa wageni!” Kukasemwa: ”Ee Mtume wa Allaah, ni kina nani wageni?” Akasema: ”Ni wale wanaozihuisha Sunnah baada yangu na kuwafunza nazo waja wa Allaah.”

Haafidhw Abu ´Abdillaah ametukhabarisha: Nimemsikia Abul-Hasan al-Kaariziy amesema: Nimemsikia ´Aliy bin ´Abdil-´Aziyz akisema: Nimemsikia Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam amesema:

”Yule mwenye kufuata Sunnah ni kama aliyeshika kaa la moto. Kwa mtazamo wangu hii leo ni bora kuliko kupigana upanga katika njia ya Allaah.”

Imepokelewa kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abudh-Dhwuhaa, kutoka kwa Masruuq, aliyeeleza:

”Tuliingia kwa ´Abdullaah bin Masruuq, ambaye akasema: ”Enyi watu! Yule mwenye kukijua kitu, basi akiseme. Na yule asiyekijua, basi aseme ´Allaah ndiye mjuzi zaidi`. Allaah (´Azza wa Jall) alisema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ

”Sema: ”Sikuombeni ujira wowote juu ya hili, na wala mimi si katika wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu.”[1]

[1] 38:86

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 250-254
  • Imechapishwa: 12/12/2023