Haafidhw Abu ´Abdillaah ametukhabarisha: Abul-´Abbaas al-Ma´qaliy ametuhadithia: Ahmad bin ´Abdil-Jabbaar al-´Utaaridiy ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: ´Abdur-Rahmaan adh-Dhwabbiy ametuhadithia, kutoka kwa al-Qaasim bin ´Urwah, kutoka kwa Muhammad bin Ka´b al-Quradhwiy, ambaye ameeleza:

”Niliingia kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz na nikaanza kumwangalia kwa macho makali. Akasema: ”Unanitazama mtazamo ambao ulikuwa hunitazami nilipokuwa Madiynah.” Nikasema: ”Unanishangaza.” Akasema: ”Kipi kinachokushangaza?” Nikasema: ”Juu ya kubadilika kwa rangi yako, mwili wako mwembamba na nywele zako zilizopotea.” Akasema: ”Ungelisema nini baada ya kuniona siku tatu ndani ya kaburi yangu wakati ambapo macho yangu yanatiririka kwenye mashavu yangu na pua yangu ikageuka usaha ndani ya mdomo wangu? Hapo hapo ndipo ungeshangaa zaidi. Nisimulie Hadiyth uliyokuwa ukinihadithia kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Abbaas.” Nikasema: ”´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amenihadithia, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema: ”Hakika kila kikao kina utukufu wake. Vikao vilivyojaa utukufu ni vile ambavyo mtu anaelekea Qiblah. Usiswali nyuma ya mlalaji wala mwenye hadathi. Muueni nyoka na nge hata kama mtakuwa ndani ya swalah zenu. Msifunike kuta kwa nguo zenu. Yule mwenye kutazama kitabu cha ndugu yake pasi na idhini yake basi hakika anautazama Moto. Nisikupe khabari ya waovu wenu zaidi?” Wakasema: ”Ndio, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: ”Ni yule anayempiga mtumwa wake, anamzuia asisaidiwe na anajipa ugeni mwenyewe. Nisikupe khabari juu ya ambao ni waovu zaidi kuliko huyo? Ni yule anayewabughudhi watu na wao wanambughudhi. Nisikupe khabari juu ya ambao ni waovu zaidi kuliko huyo? Ambaye hapuuzi makosa, hakubali nyudhuru wala hasamehi madhambi. Nisikupe khabari juu ya ambao ni waovu zaidi kuliko huyo? Ambaye hakutarajiwi kheri zake na wala hakuaminiwi shari zake. Yule ambaye anataka kuwa mtu mwenye nguvu zaidi basi amtegemee Allaah. Yule ambaye anataka kuwa tajiri zaidi wa watu basi ategemee yale yaliyoko mikononi mwa Allaah zaidi kuliko yale yaliyoko mikono mwa wengine. Yule ambaye anataka kuwa mtukufu zaidi wa watu basi amche Allaah. ´Iysaa (´alayhis-Salaam) alisimama kati ya watu wake na kusema: ”Enyi wana wa israaiyl! Msizungumze kwa hekima mbele ya wajinga, mkawadhulumu. Msiwanyime wenye hekima, mkawadhulumu. Msidhulumu. Msiwalipe dhuluma wenye kudhulumu, mkakosa ubora wenu mbele ya Mola wenu. Mambo ni matatu: ambalo liko kati ya busara yake; lifuateni, jengine liko kati ya upotofu wake, jiepusheni nalo; na jengine ambalo mmekhitilafiana; basi mwachieni nalo Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

[1] Dhaifu sana kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1672).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 254-256
  • Imechapishwa: 12/12/2023