Mazungumzo ya kidunia msikitini

Swali: Vipi kuhusu mazungumzo ya kidunia msikitini?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa ni mazungumzo machache. Hata hivyo haifai yakiwa mengi. Mazungumzo ya kidunia yakiwa madogo yanasamehewa. Mfano wa mazungumzo hayo ni kama kuuliza hali ya watoto, hali yake, fulani amesafiri au amefika? Kitu ambacho haja imepelekea kufanya hivo.

Swali: Maongezi yakiwa marefu?

Jibu: Kurefusha mazungumzo ni kitu kinachukiza.

Swali: Akemewe mwenye kufanya hivo?

Jibu: Kwa maneno mazuri na kwa njia nzuri aambiwe kuwa yanachukiza maneno hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22047/كيف-ينصح-من-يكثر-حديث-الدنيا-بالمسجد
  • Imechapishwa: 18/10/2022