Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kubeba pakiti ya sigara au anavuta sigara na anatokwa na harufu mbaya kutoka mdomoni?

Jibu: Anasihiwe na afunzwe kama mfano wa ambaye anakula kitunguu maji. Aambiwe kutoswali na watu mpaka ajisafishe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkemea anayekuja msikiti baada ya kula kitunguu maji au kitunguu saumu ili asiwaudhi watu.

Swali: Au aache kutu hichi?

Jibu: Afunzwe. Dini ni kupeana nasaha. Muislamu ni nduguye muislamu. Dini ni kupeana nasaha. Anasihiwe, aelekezwe katika kheri, aambiwe kumcha Allaah, kwamba haijuzu, kwamba ni haramu na kwamba inamdhuru katika dini, dunia yake na afya yake na anawaudhi watu wengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22042/كيف-ينصح-من-يحمل-راىحة-الدخان-بالمسجد
  • Imechapishwa: 18/10/2022