Mawalii wa Allaah hawaabudiwi pamoja na Allaah

Swali: Amesema (Ta´ala):

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

”Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”[1]

Je, ni dalili juu ya yale wanayosema kuhusu kufaa kujikurubisha kwa mawalii na kuwaomba?

Jibu: Hapana. Hapa wanasifiwa. Kwa sababu wamemwamini na wakamcha. Kama wamesifiwa ndio ina maana kuwa wanaabudiwa badala ya Allaah? Mitume pia wamesifiwa kwamba wamemwamini na wakamtii Allaah na wakafikisha ujumbe Wake. Haya ni matendo yao wao. Haijuzu kuwaomba. Amesema (Ta´ala):

فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.”[2]

[1] 10:62

[2] 72:18

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 39
  • Imechapishwa: 21/10/2021