Swali: Ni ipi hukumu ya kumpelekea maua mgonjwa au katika minasaba mingine?

Jibu: Hii ni katika desturi za makafiri na si katika desturi za waislamu. Kuwapelekea maua wagonjwa, ni katika desturi za makafiri. Haitakiwi kwa waislamu kufanya jambo hilo. Mwombee du´aa mgonjwa. Ikiwa wanataka kumnufaisha mgonjwa, wamwombee du´aa au wamfanyie matibabu. Mgonjwa hanufaiki kitu kwa maua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 13/05/2023