Matumizi ya mjamzito wakati mume hakuacha mirathi yoyote

Swali: Mwanamke mjamzito atahudumiwa vipi ikiwa mume aliyefariki hakuacha mirathi yoyote?

Jibu: Matumizi ya mtoto yanamlazimu baba yake. Atahudumiwa kwa ajili ya ile mimba na si yeye kama yeye:

وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

”Na ni lazima kwa mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa desturi.”[1]

[1] 02:233

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 12/05/2023