Romantiki katika kafara ya kumfananisha mke na mama

Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا

”… kabla ya kugusana.”[1]

Je, kilichokusudiwa hapa ni jimaa peke yake kwa maana ya kwamba inafaa kwake kuchanganyika naye lakini asifanye naye tendo la ndoa au amekatazwa yote mawili?

Jibu: Kilichokusudiwa ni jimaa. Kuchanganyika naye ni njia inayopelekea huko. Kwa hivyo anatakiwa kujiepusha kufanya hivo. Ni kwa njia ya kuchukua tahadhari.

[1] 58:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 12/05/2023