Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga makofi?

Jibu: Kupiga makofi ni katika matendo kabla ya kuja kwa Uislamu. Haitakikani. Ikihitajika basi watu walete Takbiyr kama inavofanywa ndani ya swalah ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kupiga makofi ni kwa wanawake na Tasbiyh ni kwa wanaume.”

Isitoshe Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً

“Na haikuwa swalaah zao katika Nyumba isipokuwa ni miluzi na kupiga makofi.”[1]

Wanazuoni wamesema kuwa (المكاء) ni kupiga miluzi na (التصدية) ni kupiga makofi.

Swali: Kwa hiyo ni haramu?

Jibu: Dogo liwezelo kusemwa ni kwamba inachukiza. Kuna uwezekano mkubwa ikawa ni haramu. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kupiga makofi ni kwa wanawake… “

kunafahamisha kuwa sio katika matendo ya wanaume. Ni katika matendo ya wanawake au makafiri.

[1] 08:35

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23091/ما-حكم-التصفيق
  • Imechapishwa: 28/10/2023