Swali: Kuna ngazi mbalimbali za kujifananisha [na makafiri]? Kuna aina ambayo inachukiza na aina nyingine ambayo ni haramu?

Jibu: Ndio, ni aina mbalimbali. Mfano wa Hadiyth inayosema kuwa mayahudi hawapaki hina mvi zao na hivyo jitofautisheni nao. Inatambulika kuwa kupaka hina mvi ni jambo linalopendeza. Maeneo mengine amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawavai viatu [wakati wa kuswali] na hivyo vaeni. Kwa kifupi ni kwamba kuna aina ya kujifananisha ambayo ni haramu, kama mfano wa kujifananisha nao katika sikukuu zao, kufuru yao, upotofu wao na kuyatukuza makaburi. Aina hii ni ya maovu. Kuna sampuli nyingine ya kujifananisha ambayo iko chini ya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23092/ما-درجات-التشبه-بالكفار-وحكمها
  • Imechapishwa: 28/10/2023