Swali: Je, wanapata thawabu kutokana maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Simameni hali ya kuwa mmesamehewa kutoka katika vikao vyenu vya kumtaja Allaah?”

Jibu: Hapana shaka. Wanashukiwa na utulivu, wanafunikwa na rehema, wanazungukwa na Malaika na Allaah anawataja kwa wale walioko Kwake. Hizi ni fadhilah kuu. Rehema inawazunguka na Allaah anawataja kwa wale walioko Kwake. Allaah atujaalie sisi na nyinyi kuwa miongoni mwao. Hii ni fadhilah Yake (´Azza wa Jall). Lakini muhimu ni mtu kumtakasia nia Allaah juu ya hilo, kuwa mkweli na kutojionyesha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23093/معنى-قوموا-مغفورا-لكم-لمجالس-الذكر
  • Imechapishwa: 28/10/2023