Maswali kadhaa kuhusu kuanza kufunga baada ya tarehe 15 Sha´baan

Swali: Vipi kuhusu kufunga swawm inayopendeza baada ya nusu Sha´baan?

Jibu: Ikiwa hakuanza kufunga katika ile nusu ya kwanza, basi asifunge nusu iliyobakia.

Swali: Nakusudia swawm ya kujitolea yoyote?

Jibu: Hapana neno akaendelea kufunga jumatatu na alkhamisi. Ikiwa ana mazowea ya kufunga jumatatu na alkhamisi hapana neno.

Swali: Swawm ya masiku meupe?

Jibu: Swawm ya masiku meupe inaanza kabla ya nusu ya kwanza.

Swali: Vipi kwa mfano akiichelewesha?

Jibu: Hapana, swawm ya masiku meupe inakuwa tarehe 13, 14 na 15. Hizi ndio tarehe za swawm ya masiku meupe.

Swali: Akianza kunuia baada ya tarehe 15?

Jibu: Hapana, asianze. Kutokana na Hadiyth:

“Sha´baan inapofika katikati, msifunge.”

Swali: Kama alifunga siku moja katika nusu ya kwanza ya Sha´baan aendelee kufunga nusu ya pili?

Jibu: Udhahiri wake ni kwamba haina neno. Kama alianza kufunga siku kadhaa kabla yake hapana vibaya akaendelea. Muhimu ni yeye afunge siku nyingi za Sha´baan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22826/ما-حكم-صوم-التطوع-بعد-انتصاف-شعبان
  • Imechapishwa: 28/08/2023