Swali: Ikiwa nina ndugu yangu muislamu kwa ajili ya Allaah au jamaa ambaye daima ananishambulia, ananitukana na ananidhulumu bila sababu. Kila ninapomsusa na kumrejea anarudi kufanya hayohayo. Je, niendelee kumkata ikiwa nasaha hazifui dafu?

Jibu: Ukiweza kumshauri ndio bora zaidi. Mnasihi pengine Allaah akamwongoza. Ikiwa kuwasiliana naye kunapelekea katika shari, basi usiwasiliane naye. Ikiwa ni mtu mbaya na fasiki ambaye hajali na nasaha kwake hazinufaishi kitu, msuse.

Swali: Hakuzingatiwi ni kukatana na kuchukiana kati ya waislamu wawili?

Jibu: Hapana, hakuna dhambi. Yeye ndiye dhalimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22829/حكم-قطيعة-القريب-الموذي-بعد-نصحه
  • Imechapishwa: 28/08/2023