Swali: Watu wengi wa leo wanadharau kusoma masomo ya Dini na wanasema watu wenye vyeti dhaifu au akili ndogo ndio waende kusoma kitivo cha Shari´ah. Vipi tutawaraddi watu hawa ambao wamekuwa wengi? Vijana wengi wamekuwa wanakimbia kitivo cha masomo ya Dini kwa kuwa hayana maisha ya mbele.

Jibu: Watu hawa ima ni wajinga na hawajui lolote juu ya masomo au ni wapotevu. Wanajua, lakini wanapoteza. Hawataki watu wasome elimu yenye manufaa na vitivo vya Shari´ah. Wanasema wazembe tu na vigugu ndio husoma huko na hayana maisha ya mbele.

Je, mmeona wanafunzi kuwa ni wazururaji wasiokuwa na kazi? Wao ndio majenerali sasa. Wao ndio walinganizi, waalimu na wenye kuhukumu. Hili ni jambo liko wazi kabisa. Mtu mwenye kutafuta elimu ya Dini ametukuka na yujuu. Hakosi nafasi katika jamii. Hili ni katika jamii ambazo sio za Kiislamu na nchi ambazo haziutaki Uislamu. Katika nchi ya Kiislamu mwanafunzi ametukuzwa na anaheshimiwa Watu wanamuhitajia, wanamuuliza na wanaomba ushauri kwake. Ni wajibu kwa mwanafunzi amjengee dhana nzuri Allaah (´Azza wa Jall) na atafute elimu ya Kishari´ah. Asiwe na wasiwasi ya maisha ya kidunia na kazi:

وَمَنيَتَّقِاللَّـهَيَجْعَللَّهُمَخْرَجًاوَيَرْزُقْهُمِنْحَيْثُلَايَحْتَسِبُ ۚ وَمَنيَتَوَكَّلْعَلَىاللَّـهِفَهُوَحَسْبُهُ

“Na yeyote (yule) anayemcha Allaah; (basi Allaah) Atamjaalia njia (ya kutoka katika matatizo). Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote (yule) anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. Hakika Allaah Anatimiza amri Yake. Allaah Amejaalia kwa kila kitu kipimo chake.” (65:02-03)

Awe na dhana nzuri kwa Allaah (´Azza wa Jall) na aendelee katika safari yake na asiwasikilize wababaishaji na wanafiki. Kwa kuwa mwanafunzi ni mwenye kukinaika katika hali aliyomo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015