Swali: Wakati wa kufunga kwa ndoa, mwanaume ametamka kuwa amekubali kumuoa mwanamke kwa sauti ya chini kabisa kiasi cha kwamba wale mashahidi wawili hawakumsikia. Kisha baadaye wakaachana. Je, ndoa inasihi?
Jibu: Hapana. Ni lazima wasikie wale mashahidi wawili na wathibitishe hilo. Hakuna faida ikiwa hawakumsikia.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
- Imechapishwa: 05/08/2023