Mashahidi hawakusikia kukubali kwa mwanaume kumuoa mwanamke

Swali: Wakati wa kufunga kwa ndoa, mwanaume ametamka kuwa amekubali kumuoa mwanamke kwa sauti ya chini kabisa kiasi cha kwamba wale mashahidi wawili hawakumsikia. Kisha baadaye wakaachana. Je, ndoa inasihi?

Jibu: Hapana. Ni lazima wasikie wale mashahidi wawili na wathibitishe hilo. Hakuna faida ikiwa hawakumsikia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 05/08/2023