Mapendekezo ya kusimama usiku wa Qadr

Swali: Ni ipi alama za usiku wa Qadr? Ni kipi kinachompasa muislamu katika usiku huo?

Jibu: Inapendeza kusimama usiku wa Qadr. Ni usiku umewekwa maalum katika yale masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan. Zile nyusiku za witiri zina uhakika zaidi kuliko nyenginezo. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kujitahidi kumtii Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika michana na nyusiku hizi kumi. Kusimama usiku kuswali si jambo la lazima. Ni kitu kinapendeza. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijitahidi katika masiku kumi ya mwisho kuliko anavofanya katika masiku mengine. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa zinapoingia zile siku kumi za mwisho basi anahuisha usiku, anaiamsha familia yake, anakuwa jadi na hufunga vizuri kikoi chake.”[1]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayesimama kuswali usiku wa Qadr kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”[2]

Kuna Hadiyth nyingi zenye maana kama hiyo.

[1] al-Bukhaariy (1884) na Muslim (2008).

[2] al-Bukhaariy (1768) na Muslim (1268).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/431)
  • Imechapishwa: 15/04/2023