Swali: Tumesoma katika darsa iliyopita ya kwamba wakati mwanamke anapotoka kwenye hedhi atumie manukato. Je, kuna manukato maalum kwa vile kuna baadhi ya manukato ambayo bei yake ni ghali sawa na Riyaal 1000 na mengine Riyaal 30? Je, kuna mpaka katika Sunnah?

Jibu: Muhimu atumie manukato mazuri ambayo yataondosha harufu ya hedhi, ni mamoja yakiwa ni bei ghali au bei nafuu. Lililo muhimu ni yeye aondoshe harufu ya hedhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-09.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020