Swali: Msichana wangu mdogo huuliza siku zote ni kwa nini hatumuoni Allaah duniani. Ni njia ipi bora ya kumjibu kwa kuzingatia ya kwamba bado ni mdogo?

Jibu: Mwambie ni kwa sababu hatuna uwezo wa kufanya hivo. Tunaweza kuchomeka. Viumbe hawawezi kumuona Allaah duniani. Ama kuhusu Aakhirah, Allaah Atawapa waumini nguvu na wataweza kumuona Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-09.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020