Maneno ya Mtume au maneno ya mwanafunzi?

Swali: Kuhusiana na kuwauza mbwa waliyopewa mafunzo, wako baadhi ya wanafunzi wanaosema kuwa kinachofaa ni ile thamani ya mafunzo na sio mbwa mwenyewe…

Jibu: Hizi ni hila. Ni hila na haisilihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza biashara ya mbwa. Kisha anakuja mtu na kusema kuwa ni halali na kwamba ni thamani ya mafunzo ndio yenye kuuzwa? Sio thamani ya mafunzo kabisa inayouzwa, ni mbwa  mwenyewe. Imekuja katika Hadiyth:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza thamani ya mbwa… ”[1]

Iko wazi.

[1] al-Bukhaariy (2237).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 09/12/2023