02. Hadiyth “Anayekula kutoka katika mti huu basi asitukurubie… “

332 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن أكلَ من هذه الشجرةِ فلا يقربَنّا، ولا يصلِّيَنَّ معنا

“Anayekula kutoka katika mti huu basi asitukurubie na wala asiswali nasi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Imekuja kwa at-Twabaraaniy:

إياكم وهاتَين البَقْلَتيْن المُنْتِنَتَيْن أنْ تأكلوهما، وتدخلوا مساجدَنا، فإنْ كنتُم لا بدَّ آكليهما فاقتلوهما بالنار قَتْلاً

“Jihadharini na mimea miwili hii ya mboga inayonuka vibaya mkaila na mkaingia misikiti yetu. Ikiwa mnalazimika kuila, basi iueni kwanza kwa moto.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/254-255)
  • Imechapishwa: 09/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy