Swali: Suala la maadili ni suala linalomhusu kila muislamu. Kwa hiyo ni njia zipi zinazosaidia kupata maadili haya? Vipi kuhusu subira ya kuyatekeleza ikiwa tayari yapo kwa muislamu?
Jibu: Sababu kubwa zaidi ni kumuomba Állaah du´aa na kumlilia Yeye akuwafikishe katika jambo hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ee Allaah! Niongoze katika maadili bora kabisa, hakuna wa kuniongoza kwenye yaliyo bora isipokuwa Wewe. Uniondolee maadili mabaya, hakuna wa kuniondolea isipokuwa Wewe.”
Hivyo humuomba Mola wake amsaidie kupata maadili mema na matendo mazuri. Hii ndiyo sababu ya kwanza na kubwa zaidi.
Sababu ya pili ni kutafuta elimu na kupata ufahamu, kuyajua maadili mema na kuyajua maadili mabaya yaliyochafuliwa ili ayazoe maadili mema na ajiepushe na maadili mabaya.
Sababu ya tatu ni kushikamana na watu wema na kuwa na usuhuba nao. Sambamba na hilo kujiepusha na watu waovu, kwani hii ni miongoni mwa sababu kubwa za kujipamba na maadili mema na kujiepusha na maadili mabaya.
Sababu ya nne ni kujitahidi na kuipiga vita nafsi. Lazima pawe na jihadi na subira. Ni lazima ajilazimishe kwenye maadili mema na ajihadhari kwa nguvu zake zote, kwa bidii zake zote na kwa uwezo wote aliopewa na Allaah dhidi ya maadili mabaya. Hivi ndivyo alivyo muumini. Sababu hii ya nne inahitaji subira na kuvumiliana. Nafsi haipati mambo kwa urahisi, si kwa wepesi. Ni lazima kuwe na subira na jihadi dhidi ya nafsi ili izoe maadili mema, isimame juu yake na ijiepushe na maadili mabaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2217/الوساىل-المعينة-على-اكتساب-الاخلاق-الحميدة
- Imechapishwa: 18/07/2026
Swali: Suala la maadili ni suala linalomhusu kila muislamu. Kwa hiyo ni njia zipi zinazosaidia kupata maadili haya? Vipi kuhusu subira ya kuyatekeleza ikiwa tayari yapo kwa muislamu?
Jibu: Sababu kubwa zaidi ni kumuomba Állaah du´aa na kumlilia Yeye akuwafikishe katika jambo hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ee Allaah! Niongoze katika maadili bora kabisa, hakuna wa kuniongoza kwenye yaliyo bora isipokuwa Wewe. Uniondolee maadili mabaya, hakuna wa kuniondolea isipokuwa Wewe.”
Hivyo humuomba Mola wake amsaidie kupata maadili mema na matendo mazuri. Hii ndiyo sababu ya kwanza na kubwa zaidi.
Sababu ya pili ni kutafuta elimu na kupata ufahamu, kuyajua maadili mema na kuyajua maadili mabaya yaliyochafuliwa ili ayazoe maadili mema na ajiepushe na maadili mabaya.
Sababu ya tatu ni kushikamana na watu wema na kuwa na usuhuba nao. Sambamba na hilo kujiepusha na watu waovu, kwani hii ni miongoni mwa sababu kubwa za kujipamba na maadili mema na kujiepusha na maadili mabaya.
Sababu ya nne ni kujitahidi na kuipiga vita nafsi. Lazima pawe na jihadi na subira. Ni lazima ajilazimishe kwenye maadili mema na ajihadhari kwa nguvu zake zote, kwa bidii zake zote na kwa uwezo wote aliopewa na Allaah dhidi ya maadili mabaya. Hivi ndivyo alivyo muumini. Sababu hii ya nne inahitaji subira na kuvumiliana. Nafsi haipati mambo kwa urahisi, si kwa wepesi. Ni lazima kuwe na subira na jihadi dhidi ya nafsi ili izoe maadili mema, isimame juu yake na ijiepushe na maadili mabaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2217/الوساىل-المعينة-على-اكتساب-الاخلاق-الحميدة
Imechapishwa: 18/07/2026
https://firqatunnajia.com/mambo-yatayokusaidia-kuwa-na-maadili-mema/