Swali: Baba yangu anatumia ugoro na hunituma nikamnunulie ugoro huu. Je, ni katika kumtendea wema nikitii ilihali ninajua kuwa huenda akakasirika nisipomnulia?
Jibu: Uvutaji wa tumbaku kwa aina zake zote ni haramu. Kwa hivyo haijuzu kusaidia katika hilo na ugoro ni aina yake. Haijuzu kusaidia katika aliyoharamisha Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametuhalalishia vizuri na ametuharamishia vibaya. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ
“Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: “Mmehalalishiwa vilivyo vizuri.”[1]
Kwa hiyo Allaah ametuhalalishia vizuri tu. Madaktari waliobobea katika tumbaku na wengineo wanaoifahamu wameafikiana kuwa tumbaku si katika vizuri, bali ni katika maovu yaliyoharamishwa. Ndani yake kuna madhara mengi yaliyobainishwa na madaktari na yanayojulikana kwa wanaoitumia. Kwa hiyo haijuzu kwa mtoto kumsaidia baba yake katika aliyoyaharamisha Allaah, si katika pombe, tumbaku, zinaa, kamari wala mengineyo. Lakini ni juu yako kumjibu kwa maneno mazuri na tabia njema na kumweleza kwa njia ya upole ya kwamba vinamdhuru na kwamba haijuzu na kwamba haijuzu kwako kumtii katika lisilo haki. Hakika utiifu ni katika mema, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mweleze kwamba huwezi kumtii katika jambo hili. Ama ukilifanya mwenyewe, basi hilo ni juu yako na ninamuomba Allaah akuafikishe kuacha na akusaidie kuliacha. Yote haya yasemwe kwa maneno mazuri na mtindo mwema. Huenda ukawa sababu ya uongofu, si kwa ukali wala kwa ususuwavu.
[1] 05:04
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2208/حكم-طاعة-الوالد-في-شراء-الدخان-له
- Imechapishwa: 18/07/2026
Swali: Baba yangu anatumia ugoro na hunituma nikamnunulie ugoro huu. Je, ni katika kumtendea wema nikitii ilihali ninajua kuwa huenda akakasirika nisipomnulia?
Jibu: Uvutaji wa tumbaku kwa aina zake zote ni haramu. Kwa hivyo haijuzu kusaidia katika hilo na ugoro ni aina yake. Haijuzu kusaidia katika aliyoharamisha Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametuhalalishia vizuri na ametuharamishia vibaya. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ
“Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: “Mmehalalishiwa vilivyo vizuri.”[1]
Kwa hiyo Allaah ametuhalalishia vizuri tu. Madaktari waliobobea katika tumbaku na wengineo wanaoifahamu wameafikiana kuwa tumbaku si katika vizuri, bali ni katika maovu yaliyoharamishwa. Ndani yake kuna madhara mengi yaliyobainishwa na madaktari na yanayojulikana kwa wanaoitumia. Kwa hiyo haijuzu kwa mtoto kumsaidia baba yake katika aliyoyaharamisha Allaah, si katika pombe, tumbaku, zinaa, kamari wala mengineyo. Lakini ni juu yako kumjibu kwa maneno mazuri na tabia njema na kumweleza kwa njia ya upole ya kwamba vinamdhuru na kwamba haijuzu na kwamba haijuzu kwako kumtii katika lisilo haki. Hakika utiifu ni katika mema, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mweleze kwamba huwezi kumtii katika jambo hili. Ama ukilifanya mwenyewe, basi hilo ni juu yako na ninamuomba Allaah akuafikishe kuacha na akusaidie kuliacha. Yote haya yasemwe kwa maneno mazuri na mtindo mwema. Huenda ukawa sababu ya uongofu, si kwa ukali wala kwa ususuwavu.
[1] 05:04
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2208/حكم-طاعة-الوالد-في-شراء-الدخان-له
Imechapishwa: 18/07/2026
https://firqatunnajia.com/mzazi-anapokutuma-kumnunulia-tumbaku/