Eda ya mwanamke ambaye ameachwa kabla ya kuingiliwa na mumewe

Swali: Kama mwanamke alikuwa kwa mume wake miaka mitatu na hakuwahi kulala naye kwa sababu alikuwa anamchukia, kisha baada ya muda baba yake akaomba hati ya talaka na akamrudishia mahari aliyolipa. Je, mwanamke huyu ana wajibu wa kukaa eda baada ya talaka ilihali alikuwa amekaa kwa baba yake muda wa miaka mitatu na hakuwahi kulala naye na wala hakupata mimba?

Jibu: Kama alijivua katika ndoa kwa sababu ya kumchukia mume wake na kushindwa kuendelea kuishi naye, kisha wakakubaliana juu ya kujivua na wakamrudishia mahari yake au sehemu ya mahari au chochote na wakakubaliana juu ya hilo na mume akamtaliki kwa kubadilishana na mali, basi kwa mujibu wa maoni sahihi inamtosha hedhi moja tu. Haimlazimu eda kamili ya hedhi tatu. Mwanamke aliyejitoa ndani ya ndoa kwa kujivua imethibiti katika Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimruhusu kusubiri hedhi moja tu na akaifanya hiyo iwe tosha. Kwa sababu yeye ni kama aliyojinunua nafsi yake, kama kijakazi aliyejitoa. Kwa hiyo kwake inatosha hedhi moja tu kama uthibitisho wa kuwa tumbo lake halina mimba na hiyo inatosha. Kama atasubiri hedhi tatu kwa kutoka katika tofauti ya wanazuoni, basi hilo ni bora zaidi kabla ya kuolewa tena. Lakini kwa mujibu wa maoni sahihi katika kujivua, khaswa aliyetalikiwa kwa mali, yaani mumewe amemtaliki kwa kubadilishana na mali kwa sababu ya hali mbaya kati yao, basi eda yake ni hedhi moja tu. Isipokuwa kama ni mjamzito, basi eda yake ni mpaka ajifungue, kama inavyojulikana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2175/عدة-المخالعة-التي-لم-يدخل-بها-زوجها
  • Imechapishwa: 17/07/2026