Ikiwa binti wa ndugu yangu amenyonyeshwa na mke wangu dada zake wanakuwa haramu kwa watoto wangu?

Swali: Binti yangu amenyonyeshwa na mke wa ndugu yangu na binti wa ndugu yangu pia amenyonyeshwa na mke wangu. Je, inaruhusiwa kwa wana wa ndugu yangu wengine kuwaoa wasichana zangu wengine na vivyo hivyo kinyume chake?

Jibu: Ikiwa binti wa ndugu yako alinyonya kutoka kwa mke wako unyonyeshaji wa Kishari´ah mara tatu au zaidi, basi unyonyeshaji huo humharamisha kwa wana wako na yeye anakuwa dada yao. Ikiwa alinyonya ndani ya miaka miwili mara tano au zaidi kutoka kwa mke wako, basi wana wako wote hawaruhusiwi kumuoa, lakini hakuna tatizo wao kuwaoa dada zake ambao hawakunyonyeshwa.

Vivyo hivyo ikiwa binti yako alinyonya kutoka kwa mke wa ndugu yako, basi amekuwa binti wa ndugu yako. Ikiwa unyonyeshaji ulikuwa mara tano au zaidi ndani ya miaka miwili, basi anakuwa binti wa ndugu yako na imeharamishwa kwa watoto wake kumuoa. Lakini hakuna tatizo kwa watoto wa ndugu yako kuwaoa wasichana zako wengine, wakamuona yule ambaye hakunyoka kutoka kwa mke wa ndugu yako. Hivyo inapaswa kueleweka kwamba yule aliyenyonya kutoka kwa mke wa ndugu yako haruhusiwi kwa watoto wako, na yule aliyenyonya kutoka kwa mke wako pia haruhusiwi kwa watoto wa ndugu yako.

Kwa ufupi binti wa ndugu yako aliyenyonyeshwa pamoja na watoto wako amekuwa binti yako na ameharamishwa kwa watoto wako, binti yako aliyenyonyeshwa na mke wa ndugu yako amekuwa binti wa ndugu yako na haruhusiwi kwa watoto wake na wengine waliobaki hakuna tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2219/اذا-رضعت-ابنة-اخي-من-زوجتي-فهل-تحرم-اخواتها-على-اولادي
  • Imechapishwa: 17/07/2026