Huyu ni mjinga zaidi kuliko ngamia, ng´ombe na ngamia wa kufugwa

Swali: Picha kutoka katika gazeti miongoni mwa majarida, ukurasa wa 16, chini ya mada “Tukio katika Chuo cha Shari´ah”. Ufupisho wa yaliyomo katika jambo hili kwamba mmoja wa maprofesa wa Chuo cha Shari´ah, naye ni Dr. Hasan Haytu ambaye amesema:

”Hakika anayepinga maafikiano ya ummah wa Kiislamu basi yeye ni kafiri na kwamba Ibn Taymiyyah ni mmoja wa wanazuoni wa Shaam aliyepinga maafikiano ya ummah. Lau asingekufa akiwa gerezani, basi angetekelezewa adhabu ya kuritadi.”

Kwa hiyo tunaomba kutoka kwa uadilifu wenu mtukufu mtupatie maoni juu ya jambo hili au majibu anayesema maneno kama haya katika vyombo vya khabari vya Kuwait.

Jibu: Haya ndiyo tuliyoyasikia. Anayesema haya, basi yeye ni mjinga kuliko punda wa kufugwa. Anayesema maneno haya, ni mamoja iwe ni Hasan, si Hasan, Dr au mtu mwengine, anayesema mfano wa maneno haya basi yeye ni mpotofu kuliko ngamia wa kufugwa na ng’ombe wa kufugwa. Hakuna shaka kwamba amesema pasi na elimu na amesema maneno ya kiharibifu na ya kipotofu.

Hakika Ibn Taymiyyah hakupinga maafikiano ya ummah. Bali alibainisha yale yanayopasa ummah kuyachukua, akafafanua masuala ambayo watu walikhitalifiana na akaweka wazi moja ya maoni mawili yaliyo na nguvu zaidi miongoni mwa maoni mawili au miongoni mwa maono. Alifanya hivo kwa dalili. Yeye si katika wanaopinga maafikiano ya ummah, bali ni katika wanaolingania kheri na wanaokataza uovu. Lakini ameenda kinyume na masuala ya wengi katika ummah. Kipimo ni dalili, hata kama iko pamoja na wachache. Ikiwa wengi wako juu ya maoni na wachache miongoni mwa wanazuoni wako juu ya maoni mengine na wakati huohuo dalili iko pamoja na wachache, basi haki iko pamoja na wachache. Haki iko pamoja na yule aliye na dalili, hata kama wao ni wachache miongoni mwa wanazuoni. Haki haiko pamoja na wengi; haki iko pamoja na yule aliye na dalili. Yeyote aliyesimama juu ya dalili kutoka katika Qur-aan au Sunnah, basi huyo ndiye mwenye haki hata kama wanaosema hivyo si wengi, bali ni wachache.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2220/الرد-على-من-قال-ان-ابن-تيمية-خالف-الاجماع
  • Imechapishwa: 17/07/2026