Swali: Kuna mtu aliingia msikitini akaanza swalah ya kujitolea, kisha swalah ikakimiwa kabla hajarukuu. Je, atoe salamu au aikamilishe kwa kuiwepesisha?
Jibu: Kwa hali yoyote anayekwishaanza swalah ya kujitolea kisha swalah ikakimiwa, basi anaikatiza. Kwa sababu swalah ya faradhi ni muhimu zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Swalah inapokimiwa, basi hakuna swalah isipokuwa ile iliyo faradhi.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh”.
Basi lililo wajibu kwa anayekwishaingia katika swalah ya kujitolea – ni mamoja iwe ni swalah ya mamkuzi ya msikiti au Raatibah – kisha swalah ikakimiwa, basi anatakiwa kuikata swalah hii ya kujitolea. Kwa maana anuie kukata na ajishughulishe na swalah ya faradhi pamoja na imamu. Isipokuwa ikiwa yuko mwisho wake na tayari ameenda katika Rukuu´ ya pili, basi jambo hili ni lenye wasaa. Ikiwa yuko mwisho wake, basi kilichobaki si Rak´ah kamili, bali ni kitu kidogo, jambo ambalo halimzuii kumfuata na kumdiriki imamu kuanzia mwanzo wa swalah.
Kwa hiyo ikiwa swalah itaanza naye yuko katika Rukuu´ ya pili, katika sijda ya mwisho au katika Tashahhud, basi aikamilishe, kisha amfuate imamu. Kwa sababu kiasi cha swalah ni Rak´ah. Ikiwa ameenda Rukuu´ ya pili, basi kilichobaki ni chini ya Rak´ah. Katika hali hiyo anakamilisha, kisha anajiunga na imamu.
Mwanafunzi: Je, hii ni katika Rak´ah ya kwanza?
Ibn Baaz: Anaikata katika Rak´ah ya kwanza au ya pili. Anaikata ikiwa ni kabla ya Rukuu´. Hili ndilo linalopasa kwa ujumla wa Hadiyth:

Kiwango cha chini cha swalah ni Rak´ah. Basi ikiwa amebakiwa na Rak´ah, basi anaikata.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2221/حكم-من-شرع-في-النافلة-ثم-اقيمت-الصلاة
- Imechapishwa: 17/07/2026
Swali: Kuna mtu aliingia msikitini akaanza swalah ya kujitolea, kisha swalah ikakimiwa kabla hajarukuu. Je, atoe salamu au aikamilishe kwa kuiwepesisha?
Jibu: Kwa hali yoyote anayekwishaanza swalah ya kujitolea kisha swalah ikakimiwa, basi anaikatiza. Kwa sababu swalah ya faradhi ni muhimu zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Swalah inapokimiwa, basi hakuna swalah isipokuwa ile iliyo faradhi.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh”.
Basi lililo wajibu kwa anayekwishaingia katika swalah ya kujitolea – ni mamoja iwe ni swalah ya mamkuzi ya msikiti au Raatibah – kisha swalah ikakimiwa, basi anatakiwa kuikata swalah hii ya kujitolea. Kwa maana anuie kukata na ajishughulishe na swalah ya faradhi pamoja na imamu. Isipokuwa ikiwa yuko mwisho wake na tayari ameenda katika Rukuu´ ya pili, basi jambo hili ni lenye wasaa. Ikiwa yuko mwisho wake, basi kilichobaki si Rak´ah kamili, bali ni kitu kidogo, jambo ambalo halimzuii kumfuata na kumdiriki imamu kuanzia mwanzo wa swalah.
Kwa hiyo ikiwa swalah itaanza naye yuko katika Rukuu´ ya pili, katika sijda ya mwisho au katika Tashahhud, basi aikamilishe, kisha amfuate imamu. Kwa sababu kiasi cha swalah ni Rak´ah. Ikiwa ameenda Rukuu´ ya pili, basi kilichobaki ni chini ya Rak´ah. Katika hali hiyo anakamilisha, kisha anajiunga na imamu.
Mwanafunzi: Je, hii ni katika Rak´ah ya kwanza?
Ibn Baaz: Anaikata katika Rak´ah ya kwanza au ya pili. Anaikata ikiwa ni kabla ya Rukuu´. Hili ndilo linalopasa kwa ujumla wa Hadiyth:
”Swalah inapokimiwa, basi hakuna swalah isipokuwa ile iliyo faradhi.”
Kiwango cha chini cha swalah ni Rak´ah. Basi ikiwa amebakiwa na Rak´ah, basi anaikata.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2221/حكم-من-شرع-في-النافلة-ثم-اقيمت-الصلاة
Imechapishwa: 17/07/2026
https://firqatunnajia.com/ameanza-swalah-ya-kujitolea-kisha-kukakimiwa-swalah-ya-faradhi/