Swali: Msikiti wa zamani unaswaliwa humo, kisha ikabainika kuwa umepinda kutokana na Qiblah. Nilipotaka kurekebisha safu wakati wa swalah, ikaonekana kuwa hazinyooki na kwamba nguzo zinazuia hilo. Ni ipi hukumu?
Jibu: Ikiwa mwelekeo wa pembeni ni mdogo na haudhuru, yaani ikiwa mwelekeo wa msikiti umepotoka kidogo lakini bado unaelekea upande wa Qiblah, ingawa una mkengeuko, basi hilo halidhuru. Watu wanaswali na halidhuru swalah yao. Lakini ikiwa upindaji ni mkubwa, kwa maana umeacha upande wa Qiblah kwa mkengeuko mkali, basi hurekebishwa ama kwa upande wa jengo au kwa upande wa safu. Ama mkengeuko mdogo unasamehewa na haudhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kilicho baina ya mashariki na magharibi ni Qiblah.”
Kwa maana kwa upande wa watu wa kaskazini na kusini. Vivyo hivyo kwa watu wa mashariki na magharibi husemwa kuhusu wao:
”Kilicho baina ya kusini na kaskazini ni Qiblah.”
Ikiwa wako mashariki, basi magharibi ndiyo Qiblah chao. Kwa hiyo akipinda kutoka upande, lakini bado yuko katika mwelekeo wa magharibi, lakini anapinda kuelekea kusini au kaskazini, basi hilo halidhuru. Ama ikiwa upindaji ni mkubwa, kwa maana kwamba unakuwa karibu zaidi na upande mwingine, basi hili linadhuru swalah. Katika hali hiyo ni wajibu kurekebisha safu, kuugeuza msikiti au kuujenga upya. Ama mikenkeuko midogo husamehewa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2216/حكم-الصلاة-في-المسجد-الذي-به-انحراف-عن-القبلة
- Imechapishwa: 17/07/2026
Swali: Msikiti wa zamani unaswaliwa humo, kisha ikabainika kuwa umepinda kutokana na Qiblah. Nilipotaka kurekebisha safu wakati wa swalah, ikaonekana kuwa hazinyooki na kwamba nguzo zinazuia hilo. Ni ipi hukumu?
Jibu: Ikiwa mwelekeo wa pembeni ni mdogo na haudhuru, yaani ikiwa mwelekeo wa msikiti umepotoka kidogo lakini bado unaelekea upande wa Qiblah, ingawa una mkengeuko, basi hilo halidhuru. Watu wanaswali na halidhuru swalah yao. Lakini ikiwa upindaji ni mkubwa, kwa maana umeacha upande wa Qiblah kwa mkengeuko mkali, basi hurekebishwa ama kwa upande wa jengo au kwa upande wa safu. Ama mkengeuko mdogo unasamehewa na haudhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kilicho baina ya mashariki na magharibi ni Qiblah.”
Kwa maana kwa upande wa watu wa kaskazini na kusini. Vivyo hivyo kwa watu wa mashariki na magharibi husemwa kuhusu wao:
”Kilicho baina ya kusini na kaskazini ni Qiblah.”
Ikiwa wako mashariki, basi magharibi ndiyo Qiblah chao. Kwa hiyo akipinda kutoka upande, lakini bado yuko katika mwelekeo wa magharibi, lakini anapinda kuelekea kusini au kaskazini, basi hilo halidhuru. Ama ikiwa upindaji ni mkubwa, kwa maana kwamba unakuwa karibu zaidi na upande mwingine, basi hili linadhuru swalah. Katika hali hiyo ni wajibu kurekebisha safu, kuugeuza msikiti au kuujenga upya. Ama mikenkeuko midogo husamehewa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2216/حكم-الصلاة-في-المسجد-الذي-به-انحراف-عن-القبلة
Imechapishwa: 17/07/2026
https://firqatunnajia.com/msikiti-umeelekea-kinyume-na-qiblah/