Ameanzisha msikiti maeneo pengine baada ya msikiti wa zamani kuhamwa na watu

Swali: Niliteuliwa kuwa muadhini wa msikiti katika moja ya vijiji vya mbali. Baada ya muda wakazi waliokuwa kuzunguka msikiti walihama na nikabaki peke yangu nikiswali katika msikiti huo. Kisha nikalazimika baada ya hapo kuanzisha msikiti mpya katika sehemu nyingine karibu na wakazi na nikasimamisha humo swalah tano. Je, inajuzu kwangu katika hali hii kuacha msikiti wa zamani? Je, inajuzu kuchukua malipo yake hali ya kuwa wizara ya Awqaaf wamenizuia hilo na wakaniamrisha niswali katika msikiti ulioachwa?

Jibu: Hapana. Msikiti uliohamwa hakuswaliwi ndani yake. Kunaswaliwa katika msikiti mpya maadamu wakazi wamehama na hakuna wakazi waliobaki, basi anaswali pamoja nao katika msikiti mpya na awaswalishe humo. Msikiti wa zamani huuzwa kwa anayeuhitaji kwa matumizi mengine na thamani yake hutumika katika msikiti mwingine unaohitajika na waislamu. Huuzwa kwa anayehitaji kuufanya makazi na thamani yake hutumika katika misikiti mingine ambayo watu wanahitaji kuijenga kwa makazi mapya. Ni juu ya wizara ya Awqaaf kufanya hivyo. Ama kumwamuru abaki katika msikiti ambao hakuna mtu, hili ni kosa. Hili ni kosa kutoka kwa Awqaaf ikiwa kweli amesema aliyosema.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2235/حكم-ترك-الامامة-في-المسجد-المهجور
  • Imechapishwa: 17/07/2026