Muftiy wa Saudi Arabia na kiongozi wa Kibaar-ul-´Ulamaa´ Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh amethibitisha kwamba nusura kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kumwigiliza yeye na Sunnah zake, kuyajua maisha yake na kueneza fadhilah na mafunzo ya Uislamu.

Amesema pia kwamba yale majaribio mabaya ya kueneza filamu dhidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haidhuru unabii chochote wala Uislamu kwa hali yoyote ile. Allaah (´Azza wa Jall) amemnyanyua Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) utajo wake na akafanya utwevu kwa yule mwenye kwenda kinyume na amri yake. Amemfungulia ushindi wa wazi, amemlinda kutokamana na watu wote, amemtosheleza na wale wenye kumchezea shere, akampa mazuri zaidi na akamfanya mbaya wake ndiye mwenye kukatiliwa.

Ametilia mkazo mkubwa juu ya kwamba waislamu wanapaswa wayakemee majaribio hayo mabaya kwa mujibu wa yale yenye kuafikiana na yale aliyoyaweka Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Shari´ah. Ghadhabu zisiwafanye kuchupa mpaka yale yaliyowekwa katika Shari´ah na kuyaendea yale yaliyokatazwa na hivyo pasi na wao kujua wakawa wamefanikiwa baadhi ya malengo ya filamu hiyo. Vivyo hivyo ni haramu kuwaadhibu watu wasiokuwa na hatia, kuwashambulia ambao zimelindwa damu na mali zao na kuchoma moto na kubomoabomoa vituo vya ummah kutokana na dhambi za watenda madhambi.

Kadhalika amezihimiza nchi za ulimwenguni na mashirika ya kimataifa kumtia adabu yule mwenye kuwavulia adabu Manabii na Mitume.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alriyadh.com/net/article/768381 1433-10-28/2012-09-15
  • Imechapishwa: 28/08/2020