Swali: Mtu huyu kutoka Ufaransa anasema kuwa umetaja namna ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitangamana na wale wenye kumchezea shere Makkah. Ni vipi tutaoanisha kati ya kujitenga mbali na makafiri na kuwapendelea waongoke na kutowadhulumu?

Jibu: Hakuna mgongano wowote mpaka useme kuwa tuoanishe kitu. Sisi hatuwapendi washirikina wala mafiri. Lakini licha ya hivo hatuwadhulumu pasi na haki. Jengine ni kwamba hatulipizi kisasi ikiwa kulipiza kisasi kunapelekea katika madhara makubwa zaidi. Mambo yanatakiwa kutatuliwa kwa uangalifu na hekima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2735
  • Imechapishwa: 28/08/2020