Waislamu wanaoishi katika miji ya makafiri wanatakiwa kukemea dhuluma na mashambulizi haya kwa njia ya Kishari´ah. Waziandikie nchi na gazeti lililochapisha katuni hizo.

Kila kundi linatakiwa kuandika na wanatakiwa kuandika sana. Wanapaswa kuandika maandamano yao ya maandishi na kumwagizia waziri mkuu wa nchi hayo.

Nchi za Kiislamu pia zinapaswa kutuma maandamano hayo na kueleza kwamba Uislamu unajitenga mbali na matendo hayo mabaya. Wawarudishe mabalozi wao kutoka katika nchi ambayo katuni hiyo imechorwa na pia kuwatuma nyumbani mabalozi wa nchi hiyo.

Waislamu wachache Scandinavia na Ulaya wanatakiwa kuyatuma maandamano hayo. Hata kama wataonyesha kukereka kwao juu ya kitendo hicho wanalazimika kubaki watulivu na wavumilivu. Wasiwafanye wapumbavu katika nchi hizo wapate sababu za kuwashambulia waislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haadithatu Imtihaan Danmark li Suurat-ir-Rasuul, uk. 210-211
  • Imechapishwa: 28/08/2020