Mama anadhani kuwa yeye ndiye kamuua mwanae

Swal: Mimi ni mwanamke ambaye nalala na mtoto wangu wa kiume ambaye bado akingali mdogo. Usiku mmoja nililala naye na akawa amefariki. Nina shaka juu ya kifo chake huenda nilimlalia na huyu bado ni mdogo hawezi kustahamili ambapo akafa. Je, ni lazima kwangu kufunga? Je, mashaka haya yanazingatiwa?

Jibu: Mashaka haya hayazingatiwi na wala hayana mtazamo wowote. Nafsi zote ziko mikononi mwa Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا

“Allaah Yeye ndiye huzishika roho wakati wa kufa kwake.” (39:42)

Kuna kanuni ya Kishari´ah inayosema:

“Kimsingi ni mtu kutokuwa na dhimma.”

Mtu akiwa na mashaka juu ya jambo kama ni wajibu kwake au sio wajibu, basi kimsingi ni mtu kutokuwa na dhimma na kutokuwa na uwajibu. Kujengea juu ya hili basi tunasema ya kwamba mama huyu hakuna kinachomlazimu; si diyaa wala kafara yoyote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/722
  • Imechapishwa: 09/11/2017