Swali: Mimi ni kijana nimehifadhi Qur-aan na nina miaka kumi. Hali yangu iliendelea kuwa hivyo mpaka kipindi nilipojiwa na wakati ambapo nikawa nimepinda kutoka katika njia iliyonyooka na nikawa nimesahau Qur-aan. Hivi sasa nimetubu na sijui nifanye kipi? Unaninasihi nini? Nimetoka Jeddah kuja kusoma kwako.

Jibu: Nakupa bishara njema. Kwani hakika Allaah (Ta´ala) anawapenda watubiaji na wale wenye kujitwaharisha. Amesema (Ta´ala):

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ وَاتَّبِعُوا أَحْسَنَ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ بَغْتَةً وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ

“Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: “Msikate tamaa na  rehema ya Allaah, kwani hakika Allaah anasamehe dhambi zote; hakika Yeye ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” Rudini kila mara kutubu kwa Mola wenu na mjisalimishe Kwake kabla haijakufikieni adhabu kisha hamtonusuriwa. Fuateni yaliyo mazuri zaidi ambayo mmeteremshiwa kutoka kwa Mola wenu kabla haijakufikieni adhabu ghafla na hali nyinyi hamhisi.” (39:53-55)

Allaah amesema juu ya dhambi kubwa ambayo ni shirki. Amesema (´Azza wa Jall):

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mungu mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah ameiharamisha isipokuwa kwa haki na wala hawazini; atakayefanya hivyo atakutana na adhabu – ataongezewa adhabu maradufu siku ya Qiyaamah na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda matendo mema, basi hao Allaah atawabadilishia maovu yao kuwa mema.  Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (25:68-70)

Himdi zote anastahiki Allaah ambaye amekurudisha katika yale uliyokuwemo hapo kabla. Namuomba Allaah (Ta´ala) akuthibitishe juu yake.

Kuhusu kusahau kwako Qur-aan nadhani kwamba ikiwa utarudi kuihifadhi kwa mara ya pili itakuwa sahali kwako. Rudi kuhifadhi. Allaah atakusaidia endapo atajua kutoka kwako ukweli na ikhlaasw.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/723
  • Imechapishwa: 09/11/2017