Maliza hamu na tamaa yako ya chakula kabla ya kuanza swalah

Swali: Kuna wafungaji ambao wanaburudika kwa aina mbalimbali ya vyakula na wanachelewa mpaka kwanza wajaze matumbo yao na hivyo wanakosa sehemu ya swalah ya mkusanyiko.

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha mfungaji aanze kula kabla ya kuswali. Ni mamoja Maghrib na swalah nyingine. Mfungaji anatakiwa kuanza kwa chakula ikiwa kiko tayari. Mfungaji atayarishe ile futari aliyopata na amalize tamaa yake kisha ndio aende kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22801/حكم-التاخر-في-الطعام-حتى-تفوت-الجماعة
  • Imechapishwa: 25/08/2023