Malaika ambao hawamwachi mwanadamu katika hali yoyote

Swali: Pindi anapopata janaba muislamu mwenye janaba waislamu hawaingii pale anapokaa nyumbani na khaswa akiwa na wengine hawaingii nyumba yote?

Jibu: Sivyo. Malaika wenye kuandika na wenye kuhifadhi kamwe hawatengani naye. Lakini Malaika wenye rehema ndio ambao kwa mfano wanaweza kujitenga na sehemu ilio na sanamu kinyago au picha. Kuhusu Malaika wenye kuandika na wenye kudhibiti hawajitengi na mtu. Wao huandika mema na maovu. Vivo hivyo ndivo wanavofanya wale Malaika wenye kudhibiti. Lakini Malaika wa rehema ndio ambao wanaweza kujitenga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mko pamoja nanyi ambao hawawatengi isipokuwa wakati wa jimaa na wakati wa kukidhi haja ambapo wanaona haya.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 23/08/2019