Kumuozesha kwa nguvu mwanamke mtumzima aliye na zaidi ya miaka tisa

Swali 277: Ni ipi hukumu ya msichana ambaye ameozeshwa na baba yake bila ya ridhaa yake pamoja na kwamba ni mtumzima na tayari yuko na mume mwengine?

Jibu: Hali ikiwa kama mlivyotaja basi ndoa yake ya mwisho si sahihi. Miongoni mwa sharti za ndoa ni kuridhia kwa mume na mke. Mwanamke mtumzima (ath-Thayyib) halazimishwi na baba yake akiwa ameshapitisha miaka tisa, jambo ambalo kuna makubaliano juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 264
  • Imechapishwa: 23/08/2019