Makusudio ya walinganizi wanaolingania kwenda Motoni

Swali: Walinganizi wanaowalingania watu kwenye milango ya Moto ni waislamu ambao ni watu wa Bid´ah au ni makafiri?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa juu ya watu hawa. Maswahabah walimuuliza: “Tusifie nao, ee Mtume wa Allaah?” Akasema:

“Ni watu walio na ngozi zetu… ”

Bi maana ni katika makabila yetu, miji yetu na familia zetu pia.

“… na wanazungumza kwa ndimi zetu.”

Ni waarabu wafaswaha. Allaah amesema kuhusu wanafiki:

وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ

”Wanaposema, basi unasikiliza kauli yao.” (63:04)

Kwa kuwa ni watu wa ufaswaha na wa balagha. Hii ni fitina kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (4) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-18.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015