Swali: Je, ni sahihi wanayosema baadhi yao kwamba sifa nyingi za Allaah (Ta´ala) zimekuja katika upokezi wa njia ya mtu mmoja [Akhbaar Aahaad] na hivyo sio wajibu kwa watu wa kawaida kujifunza nayo?

Jibu: Ninaomba kinga kwa Allaah. Ni nani aliyesema hivi? Upokezi wa mtu mmoja ukisihi ni wajibu kuutendea kazi, ni mamoja katika ´Aqiydah na nyanja zingine. Zinafidisha elimu. Kwa sharti ziwe ni khabari sahihi zimethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) anasema:

“Hadiyth inaposihi, basi hayo ndio madhehebu yangu.”

“Maneno yangu yakienda kinyume na maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi chukueni maneno ya Mtume wa Allaah na achaneni na maneno yangu.”

Haijuzu kusema msemo huu. Andiko hakuna tofauti ndani yake. Maadamu andiko limethibiti hakuna nafasi ya tofauti. Wanaofanya hivi ni wapindaji na wapotevu, watu wenye kuzigeuza Sifa za Allaah na kuzifasiri kwa tafsiri za makosa.

Hakuna tofauti kati ya upokezi uliyopokelewa kwa njia ya mtu mmoja na upokezi uliyopokewa kwa njia ya watu wengi. Kila kimechosihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wajibu kukitendea kazi na kushikamana nacho bara bara. Kinachozingatiwa ni kusihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (3) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-17.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015