Swali: Wakati wanachuoni wanawapowaraddi watu wa batili wanasema kuwa nyama za wanachuoni ni zenye sumu. Ni yapi maoni yako?

Jibu: Makusudio sio mtu wala nyama yake. Makusudio ni kubainisha haki. Ikiwa yule mwenye kuraddi malengo yake ni mtu huyo, hili halijuzu. Ama ikiwa makusudio yake ni kubainisha haki na kumnasihi mkoseaji huyo, ni sawa. Ni jambo zuri.

Lakini ni wanachuoni tu ndio wenye kuraddi. Siku hizi kila mtu amekuwa anaraddi. Wanagonbana juu ni nani anayefaa kuzungumza na wanasema kuwa inahusiana na Radd. Wewe hustahiki Radd. Hujui namna ya kuraddi. Wewe makusudio yako wewe ni mtu huyo. Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015