Ni jambo lisiloepukika kwa Salafiy kutosemwa vibaya na Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Walinganizi wengi wanaitwa kwa majina kama ´Ikhwaaniy`, ´Jaamiy´ na ´Suruuriy`. Tunataka nasaha…

Jibu: Haya yote aliitwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alituhumiwa kuwa ni mchawi, kuhani, muongo na hili na lile. Maadamu mtu ameshikamana na haki na ana nia nzuri haimdhuru kitu kwa kule kutukanywa. Ni jambo lisiloepukana kwa wanafiki, watu wa batili na Ahl-ul-Ahwaa´ wamtukane. Asijali hili. Analotakiwa kujali ni lile lililo kati yake yeye na Allaah (´Azza wa Jall).

Muislamu anatakiwa kufikiria kile anachokisema. Ni mwenye kuulizwa kwa yale anayoyasema. Atahesabiwa kwayo:

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ

Hatamki kauli yeyote (ile) isipokuwa yuko karibu naye mwangalizi amejitayarisha (kurekodi).” (50:18)

Asiwazungumzie watu, kusengenya na kueneza uvumi. Yote yanaandikwa kwenye daftari lake. Ulimi ni khatari ikiwa hauchungwi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015