Swali: Baadhi ya viatu vinatengenezwa kwa ngozi ya nguruwe. Je, inajuzu kuvivaa?

Jibu: Hapana. Nguruwe ni najisi kwa dhati yake na haiwezi kamwe kutwaharika. Hata kama itadabighiwa na kuoshwa haitwahariki. Ni najisi:

أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ

“… au nyama ya nguruwe.” (06:145)

Bi maana nguruwe. Haijuzu kuvaa viatu vya nguruwe au kitu kingine. Haijuzu kuvitumia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015