Makusudio ya at-Tirmidhiy anaposema ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh”

Swali: Nini anachokusudia at-Tirmidhiy anaposema:

”Hadiyth hii ni nzuri, Swahiyh na ngeni.”?

Jibu: Wanazuoni wametaja kuwa huenda ameipokea kwa njia moja nzuri na njia nyingine Swahiyh, pengine vilevile wakati wa shaka maana yake ni nzuri au Swahiyh.

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa at-Tirmidhiy anaaposema:

”Hadiyth ni nzuri” na akanyamaza, basi mara nyingi ni dhaifu. Ni upi usahihi wa hilo?

Jibu: Hapana, ni istilahi yake – Allaah amrehemu. Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Ni jambo amelizindua Haafidhw Ibn Hajar katika maelezo ya ”an-Nukhbah”.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25221/ما-معنى-قول-الترمذي-حديث-حسن-صحيح-غريب
  • Imechapishwa: 18/02/2025