Kuna aina tatu za kusoma Tawraat na Injiyl:

1- Mtu akavisoma kwa ajili ya kutaka dalili na kufaidika navyo. Jambo hili halijuzu. Hivyo ni kwa sababu katika Qur-aan na Sunnah tayari kuna mambo yenye kumtosheleza.

2- Mtu akavisoma kwa ajili ya kutaka kujua haki iliyomo ndani yake na baada ya hapo amlazimishe yule mwenye kuviamini mwanamke au mwanaume na akambainishia makosa yao pale wanapokwenda kinyume na yale aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili halina neno. Bali ni jambo linalotakikana. Ima ikawa wajibu au ikawa imependekezwa tu.

3- Mtu akavisoma kwa lengo la kutaka kusoma tu ili kuyajua yale wanayofuata. Hana malengo ya kutumia kama dalili, kukinzana na Qur-aan na Sunnah. Wala hana malengo ya kujibu batili ya wale wenye kuviamini. Katika hali hii bora ni kutofanya hivo. Kwa sababu kunachelewa kwake akaathirika navyo na akavifanya kuwa ni vyanzo vya uongofu wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=GQjnVHST3Kc
  • Imechapishwa: 22/11/2018