Kuhusu qadhiya ya mwanamke, Uislamu ulipoweka vidhibiti maalum juu ya mwanamke vinavyokwenda kinyume na yale waliokuwa wakifuata wanawake katika jamii za kikafiri na kabla ya kuja Uislamu, ndipo wakawa wengi katika watu ambao wanajinasibisha na Uislamu wanachukia hukumu za Shari´ah zinazohusiana na mwanamke. Miongoni mwa mambo hayo ni kwamba wanataka mwanamke awe sawa na mwanaume katika mirathi, kazi mbalimbali na  mambo mengine ambayo ni maalum kwa wanaume na wala hawataki kabisa kuwe tofauti yoyote kati ya mwanaume na mwanaume. Hawataki hili. Yote haya kwa sababu wamagharibi wamewasawazisha wanaume na wanawake au wamewatanguliza mbele wanawake kabla ya wanaume. Wao wanachotaka ni kufuata mikia ya wamagharibi na mikia ya wanawake wa kikafiri na wala hawataki watofautishwe wanawake na wanaume katika mambo ambayo ni maalum kwa wanawake. Inapokuja katika mirathi hawataki mwanamke apate nusu ya mirathi ya mwanaume, hawataki diyaa yake mwanamke iwe nusu ya mwanaume, hawako radhi ushahidi wa mwanamke iwe nusu ya ushahidi wa mwanaume, kama ilivyokuja katika Shari´ah safi. Allaah ndiye ambaye kamuumba mwanamke na mwanaume na Yeye ni mjuzi zaidi (Subhanaahu wa Ta´ala) yanayosilihi kwa mwanaume na kwa mwanamke.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 117
  • Imechapishwa: 22/11/2018