Swali: Baadhi wanafanya mashindano na mafumbo yenye upotofu wa ki-´Aqiydah. Kama vile kusema ´mimi nina ardhini ambacho Allaah hana huko juu`, akikusudia kuwa yuko na mtoto au mke. Au akisema kuwa anachukia haki, akikusudia kifo. Au akisema kuwa yeye ni mkubwa na mwenye nguvu zaidi kuliko Allaah (أقوى من الله), akikusudia kwamba anapata nguvu kutoka kwa Allaah.

Jibu: Utani unatakiwa uwe pasi na upotofu. Anayefanya utani anapaswa kufanya hivo kwa haki. Asiwapotoshe watu. Mtindo huu ni mbaya. Ni lazima kuwawekea watu wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23503/حكم-الالغاز-التي-فيها-ايهام-عقدي
  • Imechapishwa: 01/02/2024